Michuano ya mchezo wa tennis ya Wimbledon imeendelea hii leo ambapo Muingereza Andy Murray alikuwa uwanjani katika raundi ya pili dhidi ya Dustin Brown raia wa Ujerumani.
Katila mchezk huo Murray ameendeleza wimbi la ushindi baada ya kumshinda Dustin Brown kwa seti 6-3 6-2 6-3 katika mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia sana.
Dustin Brown alionekana anaweza kuleta upinzani mkubwa kwa Murray kama alivyofanya kwa Rafael Nadal mwaka juzi lakink mchezaji huyo namba moja wa tennis alitulia na kumzamisha Brown.
Ukiacha Murray lakini kuna Muingereza mwingine aliyekuwa uwanjani ambaye ni Johanna Konta aliyekuwa akipambana na Donna Vekic katika mchezo ambao Johanna aliibuka na ushindi wa seti 7-6 4-6 na 10-8 katika mchezo uliochukua masaa matatu na dakika 10
0 comments:
Post a Comment