Na alanus
Nyota wa Arsenal Alex Oxlade
Chamberlain yuko katika harakati za kujiunga na Chelsea mchezaji huyu
mwenye umri wa miaka 24 atamaliza mkataba wake msimu ujao na Arsenal na
amekataa kuongeza mkataba mpya.
Chelsea imekataa kutoa tamko
lolote kuhusu hatua hiyo lakini inadaiwa kwamba tayari wamekubaliana
kuhusu fedha za uhamisho huo na wapinzani wao ili kumsajili mchezaji
huyo wa Uingereza.
Liverpool pia walikuwa wakimtaka mchezaji huyo na bado wanaweza kuwasilisha ombi la kuvutia ili kumnyakua mchezaji huyo.
Oxlade Chamberlain amecheza kila
mechi ya Arsenal kufikia sasa msimu huu ikiwemo kichapo cha 4-0
ilichopata Arsenal dhidi ya Liverpool wakati alipotolewa.
Kiungo huyo wa kati atakuwa
mchezaji wa 5 wa Chelsea kusajiliwa kufuatia kuwasili kwa Alvaro Morata,
kipa Willy Caballero, beki Antonio Rudiger na kiungo wa kati Tiemou
Bakayoko.
0 comments:
Post a Comment