Liverpool wacharaza Hoffenheim 4-2 na kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Liverpool
walionyesha mchezo mkali wa kushambulia na kuwazidi nguvu wapinzani wao
katika michuano ya muondoano ya kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya Jumatano na kuondoka na ushindi wa 4-2, na jumla ya
6-3.
Ushindi wao dhidi ya Hoffenheim umehakikisha kwamba kwamba
mara ya kwanza England itawakilishwa na klabu tano katika hatua ya
makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.Liverpool walikuwa wakiongoza 2-1 kutoka kwa mechi ya kwanza na walihakikisha mambo hayawezi kuwageuka kwa kufunga mabao matatu dakika 20 za kwanza za mechi.
Emre Can aliwafungia la kwanza kabla ya Mohamed Salah kuongeza la pili.
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano 23.08.2017 na Salim Kikeke
- Tetesi za soka Ulaya Jumanne 22.08.2017 na Salim Kikeke
Mshambuliaji wa zamani wa Hoffenheim, Firmino, hata hivyo alihakikisha Liverpool wanaibuka wababe kwa kufunga baada ya mapumziko Jordan Henderson alipompokonya mpira nahodha wa wapinzani wao Kevin Vogt.
Wajerumani hao, ambao walimaliza wa nne katika Bundesliga msimu uliopita, hawakufa moyo na waliokomboa bao jingine Sandro Wagner alipofunga kwa kichwa kutoka kwa krosi ya Andrej Kramaric.

Liverpool ijayo?Mechi ijayo ya Liverpool itakuwa katika Ligi ya Premia - na ni mechi kubwa.
Baada ya kwenda mechi mbili za kwanza bila kushindwa, kwa kutoka sare na Watford na kulaza Crystal Palace, watakuwa wenyeji wa Arsenal uwanjani Anfield siku ya Jumapili (16:00 BST).
0 comments:
Post a Comment