Tajiri
wa Brisbane, Meya Graham Quirk awali alishutumiwa kutoa taarifa bila
uthibitisho kutoka kambi ya Pacquiao, lakini sasa amesema kwamba
amehakikishiwa hilo katika kikao cha Jumatatu na promota wake.
"Nilikuwa
na kikao mapema leo (jana) ambacho kimrthibitisha kwamba Manny Pacquiao
atakuja mjini Brisbane mwaka huu kwa pambano la marudiano na Jeff
Horn," amesema Quirk.
Manny Pacquiao amethibitisha kurudiana na Jeff Horn mjini Brisbane baadaye mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Pambano
linatarajiwa kufanyika Novemba pale pale Uwanja wa Suncorp ambako watu
50,000 walimshuhudia mwalimu wa zamani wa shule, Horn akimshinda kwa
pointi Pacquiao kwenye pambano la raundi 12 kuwania taji la WBO uzito wa
Welter.
Pacquiao alikataa
matokeo hayo akidai mpinzani wake alipendelewa, lakini baadaye
likaundwa jopo la wataalamu kupitia upya pambano hilo ili kujua mshindi
halali, lakini ikathibitika bondia wa Ufilipino alipoteza pambano
kihalali.

0 comments:
Post a Comment