Mshambuliaji
huyo wa New York City FC, Villa aliyefunga mabao 59 ya rekodi timu ya
taifa ya Hispania, alitangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya
Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, akifunga kwa mara ya
mwisho katika mechi dhidi ya Australia, huku timu yake ikivuliwa
ubingwa wa Dunia kwa kutolewa mapema tu kwenye hatua ya makundi.
David
Villa amerejeshwa kwenye kikosi cha Hispania kwa ajili ya michezo ya
kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Italia na Liechtenstein PICHA ZAIDI GONGA HAPA
“Kurudishwa kwa David, wakati wote tumesema milango haijafungwa kwa yeyote na kazi yetu ni kufuatilia uchezaji wa kila mchezaji halali, na tumekuwa tukifanya hivyo wakati wote kwa David. Kwa wakati huu tunaamini uwepo wake ni kawaida na unakubalika, tunaamini atatusaidia. Amecheza vizuri katika timu yake (New York City FC) na mbali na hayo, tumeona ana ari na nia ya kutusaidia, na ndiyo maana tumemjumuisha,”
Julen Lopetegui kocha, alipoulizwa kuhusu Diego Costa na utayari wake kwa fainali za Kombe la Dunia Urusi, alisema; “Kuhusu Diego Costa, vizuri, kijana amekuwa na kipindi tofauti safari hii, hafanyi hata mazoezi ya ushindani, pamoja na hayo kukosekana kwake ni kawaida, kwa sababu hizo. Baada ya hapo, tutaona kitakachotokea, acha tusibashiri chochote,”
Costa hajajerejea kwenye klabu yake, Chelsea baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita, kufuatia kutofautiana na kocha Mtaliano, Antoine Conte.
Na kuhusu mshambuliaji mpya wa The Blues, Marcos Alonso, kocha Julen Lopetegui amesema;
“Nilimuon Marcos live Wembley, lakini nimemuona mara nyingi na tunamjua vizuri sana. Anacheza misimu mizuri katika timu zenye mahitaj kama Chelsea. Lakini kwa kesi hii, tena, kuna wachezaji wengine ambao wanaweza kukidhi mahitaji yetu vizuri na kuendana vizuri na mfumo wetu wa uchezaji. Hiyo haimaanishi kwamba Marcos hawezi kuitwa hata baadaye. Mwishowe, maamuzi ya aina hiyo yanachukuliwa kutokana na vigezo vidogo,”

0 comments:
Post a Comment