Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limesema kuwa sababu kubwa ya mwanariadha wa Tanzania, Emmanuel Giniki kushindwa katika mashindano ya riadha ya mabingwa wa dunia mita 5,000 kulitokana na kuumia katika mzunguko wa mwisho.
Giniki
aliongoza kwa mizunguko minne katika mbio hizo zilizofanyika juzi
Jumatano jijini London, Uingereza, lakini alimaliza katika nafasi ya 13
akitumia muda wa dakika 13:32:31 nyuma ya mshindi wa kwanza, Muethiopia
Yomif Kejelcha aliyetumia 13: 21: 50 huku bingwa wa zamani wa mbio hizo
aliyeshika nafasi ya pili Muingereza, Mohamed Farah ‘Mo Farah’ akitumia
muda wa dakika 13:30.07.
Akizungumza kutoka Uingereza, katibu wa shirikisho hilo, Wilhem Gidabudai alisema: “Giniki
amejitahidi ila tatizo hakuwa na uzoefu, alikanyagwa na spikes lep ya
pili kuelekea mwisho, amepata majeraha, alipelekwa hospitali baada ya
mbio lakini yupo salama.
“Kuhusu
Gabriel Gerald Geay alikuwa na maumivu ambayo yalianza kupona na akawa
anafanya mazoezi kwa umakini sana, ila siku mbili kabla maumivu yalimzidia sana kutokana na baridi,
makocha na madaktari wa hapa kwenye ‘Sports Village’ wakaamua asikimbie
maana uwanja ulikuwa unateleza sababu ya mvua,” alisema Gidabudai.
0 comments:
Post a Comment