TIMU
ya Borussia Dortmund imekataa ofa ya Barcelona kutaka kumnunua Ousmane
Dembele kabla ya kumsimamisha kinda huyo kufuatia kutoonekana mazoezini
Alhamkisi ya jana.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa akitaja kama mchezaji
anayefaaa kumrithi Neymar, amepigwa faini na amefungiwa kufanya mazoezi
na wachezaji wenzake hadi wiki ijayo.
Baada
ya kocha wa Dortmund, Peter Bosz kuthibitisha kwamba Dembele
hakuhudhuria mazoezi Alhamisi, klabu ikatoa taarifa ikifafanua kwamba
mshambuliaji huyo ametolewa ofa na Barcelona - moja ambayo ilikataliwa
kwa sababu haiendani na uwezo wa hali ya juu wa mchezaji huyo.
"Borussia
Dortmund ilifanya mazungumzo na FC Barcelona juu ya uhamisho wa
mchezaji wa BVB, Ousmane Dembele kwenda FC Barcelona," imesema taarifa
hiyo.
"Katika
mkutano huo, wawakilishi wa FC Barcelona walileta ofa ambayo hailingani
na kiwango kikubwa cha soka ya mchezaji wala hakilingani na thamani
halisi ya sasa katika soko la wachezaji Ulaya. Pamoja na hayo, BVB
ikaikataa ofa hiyo.
"Na kwa kuwa hakuna iliyoletwa na Barcelona hadi leo, kwa sasa hakuna mchezaji atakayehamishwa kwenda FC Barcelona,".
Baadaye
Dortmund ikatoa taarifa ya pili ikielezea kitendo cha mchezaji
kutohudhuria mazoezi ya Alhamisi bila taarifa na kumpiga faini sambamba
na kumsimamisha hadi baada ya mechi ya Rielasingen Jumamosi.
Barcelona
inamtaka Dembele kama chaguo la kwanza baada ya kumuuza mshambuliaji
wake, Neymar kwenda Paris Saint-Germain kwa dau la rekodi ya dunia,
Pauni Milioni198.
Mkurugenzi
wa Usajili wa Dortmund, Michael Zorc mapema wiki hii alikanusha taarifa
kwamba dismissed Dembele amekubaliana na vipengele binafasi na
Barcelona.
Dembele
aling'ara msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Ujerumani, akifunga mabao
sita na kujipatia nafasi katika kikosi cha kwanza cha Timu Bora ya Msimu
wa Bundesliga.
Barcelona pia imetoa ofa ya Pauni Milioni 90 kwa kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho ambayo ilikataliwa Alhamisi.
Barcelona pia imetoa ofa ya Pauni Milioni 90 kwa kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho ambayo ilikataliwa Alhamisi.
0 comments:
Post a Comment