Tuesday, September 5, 2017

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi England dakika ya 59 ikiilaza Slovakia 2-1 katika mchezo wa Kundi F kufuzu Kombe la Dunia mwakani Urusi uliofanyika Uwanja wa Wembley jana usiku. Stanislav Lobotka alianza kuifungia Slovakia dakika ya tatu kabla ya Eric Dier kuisawazishia England dakika ya 37 na ushindi huo wa sita unaihakikishia Three Lions itamaliza kileleni mwa kundi hilo

0 comments:

Post a Comment