Kocha
wa West Brom, Tony Pulis jana alimuanzisha Gareth Barry dhidi ya
Arsenal akaweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KIUNGO
wa West Bromwich Albion, Gareth Barry jana amevunja rekodi ya nyota wa
zamani wa Manchester United, Ryan Giggs kucheza mechi nyingi katika Ligi
Kuu ya England.
Barry
amesema wanawe wamelazimika kutokwenda shule ili waende kumshuhudia
akicheza mechi ya kuvunja rekodi usiku wa jana dhidi ya Arsenal Uwanja
wa Emirates.
Barry,
mwenye umri wa miaka 36 sasa, jana amecheza ya 633 ya Ligi Kuu England
baada ya kuanzishwa kwenye mechi dhidi ya The Gunners.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Aston Villa, Manchester City na Everton anavunja
rekodi ya gwiji wa Wales, Giggs ambaye alicheza mechi 672 akiwa na
Manchester United.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alimzawadia Barry jezi iliyosainiwa namba 633 na klabu hiyo ikatweet baada ya mechi: "Hongera Gareth Barry kwa kucheza mechi ta rekodi katika Ligi Kuu ya England, (pongezi) kutoka kwetu sote wa Arsenal,"
0 comments:
Post a Comment