MSHAMBULIAJI Diego Costa amewasili mjini Madrid tayari kukamilisha uhamisho wake wa kurejea klabu yake ya zamani, Atletico Madrid.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Hispania, amesafiri kutoka nchini kwake, Brazil ambako alikuwa ametulia baada ya kuachana na mabingwa wa Ligi Kuu England.
Atletico imeposti kwenye ukurasa wake wa Twitter picha
ya Costa akiwa Uwanja wa Ndege wa Adolfo Suarez Madrid Barajas na
maelezo; "Atleticos, rafiki anawasalimia!" baada ya mshambuliaji huyo
kuwasili nchini Hispania.
Atletico Madrid imefikia makubaliano na Chelsea juu ya uhamisho wa mshambuliaji huyo, Costa kurejea klabu ya Hispania.
Diego Costa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Adolfo Suarez Madrid jioni ya leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Atletico
Madrid imesema kwamba Chelsea imempa ruhusa mshambuliaji huyo kusafiri
kwenda Madrid siku zijazo kufanyiwa vipimo vya afya katika kukamilisha
mkataba wa kurejea kwenye klabu yake.
Inafikiriwa
Costa atasaini kwa dau la Pauni Milioni 53 ifikapo mwezi Januari mwaka
2018, kufuatia kutofautiana na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambayo
imesababisha asitumiwe kwenye kikosi cha The Blues hadi sasa msimu huu.
Costa
ataruhusiwa kucheza Atletico ifikapo Januari, wakati klabu hiyo
itakapomaliza adhabu yake ya kufungiwa na FIFA kusajili wachezaji wapya.
Alijiunga na Chelsea kutoka Atletico Julai mwaka 2014 kwa ada ya Pauni Milioni 32 kwa mkataba wa miaka mitano.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 aliisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mawili
ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England, akifunga mabao 59 katika mechi 120
alizocheza kwenye mashindano yote.
Lakini
alijikuta anaingia kwenye matatizo na kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio
Conte, ambaye aliripotiwa kumtumia ujumbe wa maandishi kwenye simu
kwamba hayumo mipango ya timu ya msimu huu.
Mara
moja, Costa akamlalamikia Conte hadharani na kuzungumzia nia yake
kutaka kurejea Atletico, timu ambayo alijiunga nayo kwa mara ya kwanza
mwaka 2007.
Hawezi
kucheza Atletico kwa sasa kwa sababu klabu hiyo inatumikia adhabu ya
kufungiwa na FIFA kusajili wachezaji wapya hadi mwaka 2018 baada ya
kukiuka taratibu za usajili kwa kumsajili mchezaji aliye chini ya umri.
Kwa sasa, klabu hiyo inasajili wachezaji wapya, lakini hawawezi kucheza
hadi klabu imalize adhabu.
Costa hajacheza Chelsea tangu wafungwe kwenye fainali ya Kombe la FA England na Arsenal mwezi Mei mwaka huu.
Ikumbukwe,
Atletico watakuwa wenyeji wa Chelsea katika mchezo wa Kundi C Ligi ya
Mabingwa Ulaya mjini Madrid, Hispania Jumatano ya Septemba 27, mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment