Tuesday, September 26, 2017

LeBron James asema hatokubali Trump kutumia michezo kutugawanya

Nyota wa mpira wa vikapu nchini Marekani LeBron James amewapongeza wachezaji wa ligi ya soka ya Marekani NFL ambao wamefanya mgomo dhidi ya rais Donald Trump na kumtuhumu rais huyo wa Marekani kwa kutumia michezo ili kujaribu kugawanya watu.
Trump alinukuliwa akisema siku ya Ijummaa kwamba wachezaji wa ligi ya NFL ambao walishindwa kusimama wakati wa wimbo wa taifa walifaa kufutwa kazi ama kusimamishwa kwa mda.
Katika maandamano makuba wikendi iliopita , wachezaji walijibu kwa kupiga goti moja chini huku wengine wakiamua kusalia katika chumba cha maandilizi.
James aliwapongeza wachezaji hao na kusema: Ni raia wanaondesha taifa hili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 aliongezea: Sitamruhusu mtu mmoja licha ya uwezo wake kutumia michezo kama kigezo cha kutugawanya.
''Michezo ni swala la ajabu kwa kile inachoweza kumfanyia mtu yeyote. Licha ya maumbile, ukubwa, uzani, rangi , kabila ama dini watu hukutana na timu mbali na wachezaji kwa sababu ya michezo.Inawaleta watu pamoja''.
James ambaye anaichezea Cleveland Cavaliers na amewahi kushinda mataji matatu ya NBA alimfanyia kampeni Hillary Clinton, ambaye alikuwa mpinzani wa Trump wakati wa kinyang'anyiro cha urais cha mwaka 2016.

0 comments:

Post a Comment