Tuesday, September 26, 2017


Na Thomas Ng’itu
Baada ya Uongozi wa Mbeya City kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha wao wa awali, Kina Phiri hatimaye klabu hiyo imemdaka kocha Ramadhan Nsazurwimo kutoka Burundi.
Taarifa iliyotoka katika klabu hiyo , imeeleza kuwa tayari wamefanikiwa kuingia mkataba wa awali na kocha huyo kwaajili ya kukinoa kikosi hicho kwa msimu huu.
Awali ShaffihDauda.co.tz ilizinyaka kuwa kulikuwa na majina mengi yaliyoomba kuifundisha timu hiyo, hivyo kwa kocha Ramadhan kuingia mkataba na Uongozi wa Mbeya City unamaanisha kuwa amewapiga chini majina mengine yaliyokuwa mezani kwa mabosi hao.
Kocha huyo pia katika kipindi cha maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, alikuwa akikaribia kutua katika klabu ya Ndanda lakini iliibuka sintofahamu ambayo ilifanya dili hilo kupotea hivyo kutua kwake Mbeya City ni kama imeipiga bao Ndanda iliyokuwa ikimuwania kwa muda mrefu.
Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika vilabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini, pia amewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi na kocha msaidizi/kocha mkuu wa Muda(caretaker) kwa timu ya Taifa ya Malawi.

0 comments:

Post a Comment