Tuesday, September 26, 2017

 Pep Guardiola


Tottenham wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham kwa dau la £30m wakati ambapo kiungo wa kati wa Ubelgiji Moussa Dembele anauguza jereha la mguu. (ESPN)
Philippe Coutinho amesisitiza wito wake wa kutaka kuhamia Barcelona na Liverpool inapanga kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 mnamo mwezi Januari. (Sport via Mirror)
Real Madrid inapanga kumununua kiungo wa kati wa PSG Julian Draxler
 Mshambualiaji wa Manchester United
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akihusishwa na uhamisho wa Arsenal.(Daily Star via Don Balon)
Manchester United na Chelsea wote wanamsaka mshambuliaji wa Genoa Pietro Pellegri, lakini klabu hiyo hautamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 chini ya dau la £40m. (Sun)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuwapatia kandarasi mpya Marouane Fellaini, 29, na Marcus Rashford, 19, katika uwanja wa Old Trafford. (Independent)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesisitiza kuwa mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, 22, atasalia katika klabu hiyo licha ya kuivutia Arsenal.(London Evening Standard)
Everton itafanya mkutano ili kuzungumzia kumsajili mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani, 30. (TuttoMercatoWeb - in Italian)
 Kevin de Bruyne
.
Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne anajiandaa kwa mazungumzo ya kandarasi mpya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ana takriban miaka minne iliosalia katika kandarasi yake lakini meneja Pep Guardiola anataka mchezaji huyo kusalia kwa kipindi kirefu.. (ESPN)
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amefutilia mbali shaka kuhusu hatma yake ya siku za usoni katika klabu hiyo akisema kuwa hana mpango wa kuendelea kufunza ugenini(Daily Star)
 Aliyekuwa kocha wa Crystal Palace Frank de Boer
Aliyekuwa kocha wa Crystal Palace Frank de Boer anatakiwa na klabu ya Uhispania Deportivo La Coruna. (Sun)
Newcastle United inajiandaa kuanzisha mazungumzo na meneja Rafa Benitez kuhusu kuandikisha kandarasi mpya kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mkufunzi huyo na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley(The Times - subscription required)Fran Merida
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Fran Merida mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaichezea klabu ya Osasuna katika ligi ya pili ya Uhispania anasakwa na klabu ya Leeds. (sun)
Uefa imeipatia rukhsa Bayern Munich kumrudisha kipa aliyestaafu Tom Starke, 36, katika kikosi cha vilabu bingwa baada ya kumpoteza nahodha Manuel anayeuguza jeraha (ESPN)
Kiungo wa kati wa Monaco Youri Tielemans, 20, amesema kuwa alikaidi uhamisho wa kuelekea Arsenal mnamo mwezi Agosti kuhusu wasiwasi kwamba huenda akapewa muda mchache kuichezea timu hiyo.(Metro)Christian Benteke
Crystal Palace itamkosa mshambulaiji wake Christian Benteke, 26, kwa takriban wiki sita akiendelea kuuguza jereha lake la goti. (Daily Telegraph)
Leicester wamewasilisha ombi kwa Fifa kwa lengo la kukamilisha usajili wa Adrien Silva , 28, kwa dau £25m baada ya usajili wake wa siku ya mwisho kuchelewa (Daily Telegraph)
Paris St-Germain imekataa kumuongeza marupurupu ya kitita cha Yuro 100m Edinson Cavani, 30, kwa kumuachia Neymar kuipigia penalti timu hiyo. (Independent) Laurent Kolscielny
Laurent Koscielny, 32, anasema kuwa mchezaji mwenza wa Arsenal Alexis Sanchez ameahidi kuichezea klabu hiyo baada ya jaribio lake la kutaka kuondoka kugonga mwamba (Daily Express)
Kiungo wa kati wa Watford Nathaniel Chalobah, 22, atalazimika kusubiri ili kucheza nchini Uingereza baada ya kupata jeraha la goti(Daily Mail)
Beki wa kulia wa Manchester City Kyle Walker, 27, amesema kuwa anafuraha kuwa yuko timu moja na Sergio Aguero akidai kuwa ni vigumu kukabiliana na mchezaji huyo. (Guardian)

0 comments:

Post a Comment