Tuesday, September 5, 2017

KOCHA Diego Simeone amezima uwezekano wa kuhamia Inter Milan baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kufundisha Atletico Madrid. 
Murgentina huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa vigogo hao wa Italia, ambao aliwachezea kuanzia mwaka 1997 hadi 1999, lakini ameamua kujifunga na waajiri wake wa sasa. 
Simeone anapendwa mno na mashabiki wa Atletico Madrid ambao wamejenga imani kubwa kwake kufuatia kushinda taji la La Liga kama mchezaji na baadaye kocha. 
"Kocha wetu amesaini mkataba mpya ambao unamfunga Atletico Madrid kwa misimu miwili zaidi, hadi Juni 30, mwaka 2020," imesema taarifa ya Atletico.
Diego Simeone akirushwa juu na wachezaji wake baada ya kuiwezesha Atletico Madrid kutwaa ubingwa wa Hispania mwaka 2014

0 comments:

Post a Comment