Kamati Ya Sheria,
Katiba na hadhi za Wachezaji imeridhia ridhaa za timu za Simba na Yanga
kuhusu mchezaji Pius Buswita ambaye alisaini katika timu zote mbili.
Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Elias Mwanjala alisema kwamba vilabu hivyo vilikaa na kwa pamoja
vimekubaliana mchezaji ailipe klabu ya Simba fedha ambazo alizichukua.
Mwanjala alisema
kwamba kamati hiyo imebaini kuwa mchezaji anatakuwa kuirejeshea Simba
shilingi milioni 10 pamoja na ongezeko la milioni moja kama gharama za
nauli ndipo aruhusiwe kucheza ligi.
Alisema kwamba klabu
ya Simba ilihitaji kulipwa milioni 15 wakidai ndicho kiasi walichompa
lakini kamati imeangalia mkataba aliosaini mchezaji ambao unaonyesha
alisaini kwa kiasi cha shilingi milioni 10.
Aliongeza kuwa mbali
na kurejesha fedha hizo lakini kamati itampa onyo kali mchezji Pius
Buswita kwa kitendo ambacho amekifanya cha kusaini katika vilabu viwili.
Hata hivyo alidai kua
endapo vilabu hivyo visengekubaliana vyenyewe basi kamati ingekuchukua
maamuzi makali kwa wahusika kwani ndani ya usajili huo klabu ya Simba na
Mchezaji walishindwa kufuata taratibu za usajili.
0 comments:
Post a Comment