Baadhi ya
wakimbiaji wa kike wenye homoni nyingi za kiume watatakiwa kukimbia
dhidi ya wanaume au kubadili mashindano mpaka pale watakapopata
matibabu, hizi ni sheria mpya zilizotolewa na chombo cha riadha duniani.
Sheria, ambazo zitaanza kutumika tarehe 1 mwezi Novemba,zitawahusu wanawake wanaokimbia kuanzia mita 400 mpaka maili mojaMshindi wa mbiao za mita 800 kwenye michuano ya Olimpiki, Caster Semenya ni miongoni mwa watakaoathirika
Mkimbiaji wa Afrika Kusini awali alitakiwa kufanyiwa kipimo cha kubaini jinsia na wakuu wa shirika hilo laini majibu hayakuwekwa hadharani.
''Sheria hizo si kuhusu udanganyifu, ni kuhakikisha kunakuwa na michuano ynayofanyika kwa haki na umaana''Rais wa IAAF Lord Coe alieleza
akizungumza baada ya kushinda mbio za mita 800 na mita 1500 kwenye michuano ya jumuia ya madola mwezi Aprili,Semenya alisema atakimbia umbali mrefu zaidi
Sheria inasemaje?
Wanariadha wanawake wanaotaka kushindana wanalazimika kupata dawa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kuingia mashindanoni, na kuhakikisha kuwa kiwango cha homoni hizo kinashuka.
Ikiwa mwanariadha wa kike hatataka kutumia dawa, wanaweza kushindana kwenye:
- Mashindano yeyote ya kimataifa isipokuwa mbio za mita 400 na maili moja
- Michuano yeyote ambayo sio ya kimataifa
- michuano ya wanaume katika ngazi yeyote
- michuano inayohusisha watu wenye jinsia mbili
Taarifa ya IAAF imesema sheria hizo ''hazina lengo la kuwahukumu au kuhoji jinsia ya mwanariadha''.
Katika utafiti wa hivi karibuni imeonekana kuwa wanawake wenye mchanganyiko wa homoni za kiume wana uwezo mkubwa wa kukimbia zaidi ya wasio nazo.
Semenya ashinda dhahabu mbio za 800m London
Semenya aingia fainali 800m
0 comments:
Post a Comment