Liverpool itazuia
hamu yoyote kutoka kwa Real Madrid ya kutaka kumnunua mshambulaji wa
Misri Mohamed Salah, ambaye wanasema ana thamani ya £200m. (Mail)
Mkurugenzi
wa michezo wa klabu ya Roma Monchi ametetea uuzaji wa Salah kwa
Liverpool, akisisitiza kuwa klabu hiyo ya Itali haikuwa na chaguo
kutkana na matatizo ya kifedha.(Guardian)
Mkufunzi wa New York City Patrick Vieira angependelea kurudi Arsenal wakati mkufunzi Arsene Wenger atakapoondoka mwisho wa msimu huu na kuongezea kwamba yuko tayari kufunza Ulaya.(Times)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amejiandaa kumuachilia mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kuondoka mwisho wa msimu huu (Tuttosport, via Manchester Evening News)

Arsenal huenda ikashindana na wapinzani wake katika ligi ya EPL Manchester United na Chelsea kwa usajili wa kiungo wa kati wa Roma na Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29 Radja Nainggolan. (Sun)

Tottenham inataka kuwasajili wachezaji watatu wa Ureno mwisho wa msimu huu -winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins, 22, beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares, 26, na kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves, 21. (Mirror)

0 comments:
Post a Comment