Friday, April 27, 2018

Arsene Wenger

Arsene Wenger
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa tangazo lililofanywa kuhusu kuondoka kwake katika klabu ya Arsenal siku ya Jumatano baada ya takriban miaka 22 haukuwa uamuzi wake.
Ilitangazwa siku ya Jumatano kwamba raia huyo wa Ufaransa ataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu licha ya kusalia na kandarasi ya mwaka mmoja.
Akizungumza siku ya Alhamisi kabla ya kombe la nusu fainali ya ligi ya bara Ulaya dhidi ya Atlitico Madrid, Wenger alisema kuwa ''mimi huangazia kile ninachotakiwa kufanya kila siku, kwa sasa nafanya kazi kama kawaida''.
Wenger aliongezea kwamba atafanya kazi kama kawaida na kwamba hatochukua jukumu lengine kwa sasa.
Alikuwa akijibu swali moja kutoka kwa mwandishi wa Ujerumani aliyetaka kujua kwa nini alikuwa anajiondoa wakati huu kabla ya mechi kubwa.
Baadaye siku ya Jumatano Wenger alisema kuwa hakuwa na tatizo na wakati wa tangazo hilo , lakini haukua uamuzi wake.
''Baada ya kuafikiana kwamba nitaondoka, nilikuwa na raha kwa klabu kutoa tangazo hilo''.
Nataka kuweka wazi kwamba wakati wa tangazo hilo ulikuwa sawa. Arsenal imeshinda mataji 3 ya kombe la ligi ya Premia na mataji 7 ya FA ikiwemo ushindi wa mataji mawili 1998 na 2002 chini ya usimamizi wa Wenger

0 comments:

Post a Comment