Monday, October 4, 2021

 


WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Mshambuliaji Mfaransa, Anthony Martial dakika ya 43, kabla ya Andros Townsend kuisawazishia Everton dakika ya 65.
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amejikuta lawamani kwa kumuamzishia benchi mshambuliaji tegemeo, Cristiano Ronaldo kabla ya kumuingiza dakika ya 57 kuchukua nafasi ya mkongwe mwenzake, Edinson Cavani.
United wanafikisha pointi 14 baada ya mechi saba na kushukia nafasi ya tatu, nyuma ya Chelsea inayoongoza kwa pointi zake 16 za mechi saba pia, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 14 pia za mechi sita, wakati Everton sasa ni ya nne kwa pointi zake 14 pia za mechi saba.

0 comments:

Post a Comment