Argentina
wameendelea kuhangaika katika juhudi zao za kufuzu kwa Kombe la Dunia
2018 baada ya kutoka sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya wanyonge Venezuela.
Jhon Murillo aliwapatia wageni uongozi lakini bao la kujifunga kipindi cha pili liliwawezesha Argentina kuondoka na alama moja.Argentina wanashikilia nafasi ya tano katika msimamo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia katika Amerika Kusini kukiwa na mechi mbili ambazo zimesalia kuchezwa.
Nchi zinazomaliza nne za kwanza ndizo hufuzu moja kwa moja.
Atakayemaliza wa tano atacheza dhidi ya New Zealand na mshindi afuzu.
Brazil, ambao tayari wamefuzu walitoka sare 1-1 na Colombia.
Mshambuliaji wa Chelsea Willian aliwaweka Brazil mbele kabla ya mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao kusawazisha.
Kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho aliingia kama nguvu mpya dakika za mwisho upande wa Brazil.
Uruguay walipanda hadi nafasi ya pili baada ya kulaza Paraguay 2-1 nao Peru wakalaza Ecuador 2-1 na kusonga hadi nafasi ya nne.
Chile walio nafasi ya sita walilazwa 1-0 na Bolivia.
Marekani wana kibarua
Katika kundi la kufuzu la Concacaf, bao la dakika ya mwisho la Bobby Wood liliwawezesha Marekani kutoka sare 1-1 ugenini Honduras. Romell Quioto alikuwa amewaweka wenyeji mbele lakini Wood akasawazisha dakika tano kabla ya mechi kumalizika.Nchi zote mbili zinatoshana zikiwa na alama tisa baada ha ya mechi nane, lakini Marekani wamo nafasi ya nne na Honduras nafasi ya tano kutokana na tofauti ya mabao.
Nchi tatu za kwanza zinafuzu moja kwa moja.
Costa Rica walio nafasi ya pili walishindwa kujihakikishia nafasi yao ya kufuzu baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Mexico ambao tayari wamefuzu.
Panama walipanda hadi nafasi ya tatu baada ya kulaza Trinidad na Tobago 3-0.
Haki miliki ya picha Getty Images
0 comments:
Post a Comment