UTD INAWATAKA SAUL & NAINGGOLAN
Manchester United wamepania kuwasajili Saul Niguez na Radja Nainggolan kuziba nafasi ya Michael Carrick, kwa mujibu wa Daily Star .
Mashetani Wekundu walituma skauti katika mechi ambao Roma walitoa sare dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita kuangalia viungo hao wawili.
Carrick, 36, anatarajiwa kuondoka Old Trafford mwishoni mwa kampeni za msimu huu.
SPURS YAMFUKUZIA GOMES
Tottenham wanatamani kumsajili kiungo mahiri wa Barcelona Andre Gomes na kumleta kwenye Ligi Kuu Uingereza, kwa mujibu wa the Sun .
BARCA SASA YAMGEUKIA MANE
Baada ya kumkosa Philippe Coutinho, Barcelona sasa wanamfuatilia kwa karibu sana mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, kwa mujibu wa Mirror .
Miamba hao wa Catalan walishuhudia ofa zao nyingi zikikataliwa kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili lakini bado watajaribu kwa mchezaji mwingine wa Anfield.
MAN CITY YAPANGA KUZUNGUMZA NA DE BRUYNE
Manchester City wapo tayari kumtunuku mkataba mpya Kevin De Bruyne wenye thamani ya paundi 200,000 kwa wiki baada ya kiwango safi, limeripoti Mirror .
Mkataba wa Mbelgiji huyo umebakisha miaka mitatu kumalizika, lakini Pep Guardiola anatamani kumpa mkataba mwingine mpya ili kumfunga zaidi.
MAN UTD YAMFUKUZIA ZIVKOVIC
Manchester United wamemwongeza winga wa Benfica Andrija Zivkovic katika orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili, kwa mujibu wa O Jogo .
Mashetani Wekundu walituma skauti kumfuatilia Mserbia huyo katika mechi za katikati ya juma za Ligi ya Mabingwa.
LEWANDOWSKI ANATAKA KUONDOKA BAYERN
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski amemtaka wakala wake kumtafutia timu mpya uhamisho wa majira ya joto 2018, kwa mujibu wa AS .
Klabu nyingi zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Polandi, lakini kwa mujibu wa habari anapendelea kujiunga na klabu ya Real Madrid.
MULLER ANAPENDELEA KWENDA MAN UTD
Thomas Muller angependa kujiunga na Manchester United, ikiwa ataondoka Bayern Munich kutua Ligi ya Uingereza, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa na wakati mgumu Bayern na alitajwa kwenye tetesi za Arsenal, Chelsea na Liverpool majira ya joto.
CHELSEA YAMTUPIA JICHO CHIELLINI
Beki wa Juventus Giorgio Chiellini bado jaanza mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake, kwa mujibu wa Calciomercato.com .
Mkataba wa Chiellini unaisha mwisho wa msimu huu na kwa mujibu wa habari Chelsea wanaifukuzia saini yake, kwa hiyo ni habari njema kwa kocha wa zamani wa Juve, Antonio Conte.
BARCA HAWATAMRUDIA COUTINHO UHAMISHO WA JANUARI
Barcelona hawatarudi na ofa mpya kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho dirisha la uhamisho Januari, kwa mujibu wa Marca
MAN UTD YAMFUKUZIA WINGA WA ROMA
Manchester United wanajipanga kumsajili kinda wa Roma Mirko Antonucci, ambaye hajawahi kufanya mkataba rasmi kama mchezaji mkubwa, kwa mujibu wa TransferMarketWe b.
ATLETICO YAKARIBIA KUMNASA COSTA
Atletico Madrid wana tumaini la kukamilisha usajili wa nyota wa Chelsea anayetaka kuondoka Stamford Bridge, mshambuliaji Diego Costa, kwa mujibu wa Marca .
Ripoti zinadai kuwa klabu mbili hizo zipo kwenye mazungumzo kwani Costa sasa yupo tayari kurudi Ulaya baada ya kugomea Brazili.
ARSENAL BADO INAMFUATILIA JANKTO
Arsenal bado inaendelea kumfuatilia kiungo wa Udinese Jakub Jankto, kwa mujibu wa Calciomercato.com .
AC Milan na Juventus pia zimeonesha nia ya kutaka kumsajli Jankto, ambaye ameweka bayana shauku yake kucheza Ligi Kuu Uingereza.
BARCA KUMTOLEA OFA MPYA SERI
Barcelona wanajipanga kutoa ofa mpya kwa ajili ya kiungo wa Nice Jean-Michael Seri katika dirisha la uhamisho la Januari, kwa mujibu wa Sport .
Seri alivunjika moyo Barcelona waliposhindwa kukamilisha usajili wa mchezaji huyo kwa euro milioni 40 zilizokuwa zikihitajika majira ya joto, lakini sasa klabu hiyo ya Catalan imeamsha upya nia yao kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast.
MAN UTD KUTOA £100M KWA AJILI YA GRIEZMANN
Manchester United wapo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 100 kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann mwaka ujao, kwa mujibu wa Daily Star .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amehusishwa vikali na tetesi za kutaka kutua Old Trafford, lakini kufungiwa kwa klabu yake kufanya usajili kulimfanya aendelee kubaki Hispania.
MAN CITY YASAINI NYOTA KINDA WA U.S.
Beki wa kati wa Sporting Kansas City Erik Palmer-Brown atajiunga na Manchester City kwa mujibu wa Metro na Kansas City Star .
Kinda huyo wa Marekani ataondoka MLS mara mkataba wake utakapokwisha mwishoni mwa 2017, baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya Pep Guardiola.
STERLING BADO YUMO KWENYE RADA ZA ARSENAL
Winga wa Manchester City Raheem Sterling bado ni shabaha ya washindani wa Ligi Kuu Uingereza, Arsenal kwa mujibu wa Daily Mail.
Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool ambaye yupo tayari kutua London, aliripotiwa kutakiwa na Gunners kama sehemu ya dili la Alexis Sanchez.
PEP ACHAGUA BEKI MPYA WA KATI
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anatarajia kusaini beki wa Tottenham, Toby Alderweireld kama mrithi wa Vincent Kompany, kwa mujibu wa The Sun .
Wakala wa mchezaji huyo amedai kuwa beki huyo hana furaha kulingana na kile anacholipwa White Hart Lane, £50,000 kwa wiki kwa mujibu wa ripoti.
COSTA KUHAMIA MADRID
Diego Costa anayetaka kuondoka Chelsea ameihamishia familia yake Madrid katika jitihada zake kushinikiza kutua Atletico Madrid, kwa mujibu wa The Sun .
COUTINHO AUMIZWA NA DILI LA BARCA LILILOSHINDIKANA
Mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho amebaki na jeraha la moyo kufuatia mipango yake kwenda Barcelona kukwama majira ya joto, kwa mujibu wa Don Ballon .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili anahisi miamba hao wa Catalan walihitaji kufanya jitihada zaidi kwa ajili ya saini yake. Habari zinadai kuwa alipewa uhakika na uongozi wa Barca kuwa watamsajili lakini mambo yakawa kinyume.
LIVERPOOL YAPATA USHINDANI KWA VAN DIJK
Juventus itafanya mchakato wa kumsajili beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk dirisha la uhamisho wa majira ya baridi litakapofunguliwa Januari, kwa mujibu wa the Mirror .
ARSENAL YAKUBALI KUMSAJILI LEMAR
Arsenal wamekubali masharti ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco uhamisho wa Januari. Watatumia Euro milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo wa Monaco, ambaye atalipwa paundi 250,000 kwa wiki, kwa mujibu wa The Star .
MADRID YAMFUATILIA MSHAMBULIAJI WA LEIPZIG
Real Madrid wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner wanapotafuta mbinu za kuimarisha safu yao ya mashambulizi, kwa mujibu wa Jugones, via AS.
MOURINHO KUSAINI MKATABA MPYA MAN UNITED
Jose Mourinho yu mbioni kupewa mkataba mpya Manchester United kufuatia mwanzo mzuri wa msimu wa Ligi Kuu Uingereza, kwa mujibu wa habari kutoka Telegraph .
0 comments:
Post a Comment