Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara
(SDL), inatarajiwa kuanza Septemba 30, mwaka huu kwa timu kuchuana
katika viwanja vitano tofauti.
Kwa mujibu wa Ratiba ambayo
imeambatanishwa, michezo ya siku hiyo itakuwa ni kati ya Abajalo na
Cosmopolitan; Namungo na Reha kutoka Kundi A wakati kundi B kutakuwa na
mchezo kati ya Pepsi na Madini.
Kundi C kutakuwa na mchezo
kati ya Burkinafaso na Ihefu kadhalika Boma itacheza na Mkamba Rangers
huku Kundi D likikutanisha timu za Bulyanhulu na Milambo.
Katika Kundi hilo la D Mchezo
kati ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 siku ya
Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, sasa
utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili kwenye Uwanja huo huo.
Sababu za mabadiliko haya ni
kutokana na mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC kuchezwa tarehe
30.09.2017 katika uwanja huo. Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa
kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali ya uwanja ilibidi
Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika.
0 comments:
Post a Comment