Saa 5 zilizopita
Klabu ya Fenerbahce
ya Uturuki imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa
Chelsea Diego Costa kuhusu uwezekano wa kumchukua kwa mkopo.
Costa, 28, amesalia nchini Brazil na amekataa kurejea England.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alishindwa kuhama kutoka kwa mabingwa hao wa Ligi ya Premia kabla ya siku ya mwisho ya kuhama wachezaji katika ligi nyingi kuu Ulaya.
Hata hivyo, dirisha la uhamisho wa wachezaji Uturuki bado liko wazi na litafungwa baadaye leo Ijumaa.
Duru zinasema baada ya mazungumzo ya kwanza kufanyika, uwezekano wake kuhama ni finyu, lakini mazungumzo bado yanaendelea.
- Diego Costa avalia jezi ya Atletico Madrid
- Costa asema Chelsea wanamchukulia kama 'mhalifu'
- Costa anaamini Chelsea hawamtaki
- Wachezaji wa soka waliohama Ulaya - Agosti 2017
Alitaka kurejea Atletico Madrid majira ya joto lakini klabu hiyo ya Uhispania hairuhusiwi kuwasajili wachezaji kutokana na marufuku waliyowekewa hadi Januari.
Hii ina maana kwamba Costa anaweza tu kuhamia klabu hiyo Januari mwakani.
Mshambuliaji huyo hajajumuishwa kwenye orodha ya wachezaji wa Chelsea watakaoshiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment