Tuesday, October 31, 2017

Woods anasema mashindano ya wakati huu yatamrudisha katika viwango vyake

Image captionWoods anasema mashindano ya wakati huu yatamrudisha katika viwango vyake
Tiger Woods anatarajiwa kurejea tena katika mchezo wa gofu miezi nane baada ya kuandamwa na majeraha.
Atajitupa uwanjani kuanzia Novemba 30 mpaka Desemba 3.
Woods mshindi wa vikombe 14 vya kimataifa, anapona majeraha ya upasuaji wa mgongo aliyofanyiwa miaka mitatu iliyopita ambayo kwa wakati fulani alikuwa akirudia upasuaji mara kwa mara na kumfanya kuwa dhaifu.
Alijiondoa katika michuano ya Dubai mwezi Februari kwa sababu hiyohiyo.
''Ninajipanga kurejesha heshima yangu, furaha yangu na uwezo wangu kupitia mchezo ninaoupenda, alisema Woods''
Woods hajashinda taji lolote kubwa tokea mwaka 2008.

0 comments:

Post a Comment