Timu ya AC Milan
imemtimua kocha Vincenzo Montella na badala yake imempa usukani Gennaro
Gattuso kukisimamia kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Klabu hiyo
ipo katika nafasi ya 7 kwenye orodha kwenye ligi ya Serie A ikiwa na
pointi 20, 18 nyuma ya mabingwa Napoli, baada ya ushindani wa ushindi
mara mbili pekee wa ligi katika michuano yao ya nyuma.Walitoka sare ya 0-0 na Torino nyumbani siku ya Jumapili na wameshindwa mechi zao 6 kati ya 14 msimu huu.
Gattuso, ambaye alikuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan anapokea wadhifa huo kutoka kuwa msimamizi wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 19 wa klabu hiyo.
AC Milan, ambao wameshinda taji hilo la Italia mara 18 na ni mabingwa mara 7 wa Ulaya, hawajawahi kuibuka katika nafasi tatu za juu katika ligi ya Serie A tangu 2013.
Wametumia pauni milioni 205 kuwasajili wachezaji wapya tangu mfanyabiashara wa kichina Li Yonghong kuidhibiti klabu hiyo Aprili mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment