Tuesday, November 28, 2017

Lukaku na Mourinho


Barcelona watarejea kumtafuta tena kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 25, soko litakapofunguliwa tena Januari. (Don Balon).
Manchester City nao wanafikiria kuwasilisha ombi la kumtaka beki wa Real Sociedad wa miaka 26 kutoka Uhispania Inigo Martinez mwezi Januari. (Sun)
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku huenda akapigwa marufuku mechi tatu - ikiwa ni pamoja na debi ya Manchester - iwapo FA wataamua kumuadhibu mchezaji huyo wa miaka kwa 24 kwa kile kinachoonekana kuwa kama kumpiga teke beki wa Brighton Gaetan Bong. (Daily Mail)
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji amesifiwa sana na meneja wa Manchester United Jose Mourinho, licha ya kutofunga bao lolote katika mechi tisa kati ya 10 alizochezea klabu hiyo karibuni. (Guardian)
Ericksen
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema winga wa Wales Gareth Bale, 28, hatauzwa wakati wa dirisha ndogo la kuhama wachezaji Januari. (Daily Star)
Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wanapanga kuwasilisha ofa ya £80m kutaka kumchukua mshambuliaji Mfaransa anayechezea Manchester United Anthony Martial, 21, majira yajayo ya joto. (Daily Mirror)
Arsenal nao wako tayari kutathmini ofa zenye uzito za kutaka kumchukua mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 28, na viungo wa kati Mesut Ozil, 29, wa Ujerumani na Jack Wilshere, 25, wa England mwezi Januari. (Daily Express)
Anthony Martial and Jose Mourinho
Tottenham wanamfuatilia beki wa kushoto wa Bologna Adam Masina, 23, huku wakijiandaa kutafuta mchezaji wa kujaza nafasi ya beki wa England Danny Rose, 27, endapo ataondoka. Rose amehusishwa na kuhamia Manchester United. (Daily Mirror)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte ametoa wito kwa Blues kuwa na mwelekeo zaidi sokoni Januari iwapo wanataka kuendelea kuwafukuza viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City. (Daily Mail)
Paris St-Germain nao wamewasiliana na kiungo wa kati wa Ivory Coast anayechezea klabu ya Nice Jean Seri, 26, kuhusu uwezekano wake kujiunga nao. (Le Parisien)
Kiungo wa kati wa Serbia anayechezea Liverpool Marko Grujic, 21, ataondoka Anfield kwa mkopo Januari lakini kwa sharti kwamba atakwenda klabu nyingine ya England, kwa mujibu wa wakala wake. (Blic kupitia Daily Mirror)
Mke wa Robert Lewandowski, 29, ameashiria kwamba mshambuliaji huyo wa Poland anayechezea Bayern Munich anapanga kukamilishia uchezaji wake LA Galaxy. (Business Insider)
Mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bony, 28, amesema amepokea ofa kutoka klabu za nchi za nje lakini bado anataka kusalia England na kwamba sasa yuko sawa kucheza na "anaweza kucheza vyema sana kipindi kilichosalia cha msimu". (Times).
Rafael Benitez
Meneja wa Newcastle Rafa Benitez amehimiza kuwepo utulivu baada ya klabu hiyo kushindwa ligini mechi ya nne mtawalia, walipolazwa na Watford wikendi. (Daily Telegraph)
Mshambuliaji wa Brighton Tomer Hemed alipata jezi ya Zlatan Ibrahimovic baada ya klabu yake kulazwa 1-0 Old Trafford na alipakia picha yake akiwa na shati lake kwenye Instagram Jumamosi na ujumbe: "Huwa hambadilisha shati na Ztalat, shati la Zlatan hukubadilisha #zlatanfacts." (Instagram)
Klabu moja nchini Bosnia ilipaka mipira rangi ya machungwa baada ya theluji kuanguka kwa wingi uwanjani. Mipira hiyo ilikuwa ya rangi nyeupe. (SC Sport)
Winga wa Real Madrid Bale anapanga kumlipa Beyonce awatumbuize wageni wakati wa harusi yake mwaka ujao. (Wales Online)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar hulipwa pesa nyingi zaidi msimu mmoja kuliko wachezaji wote wanaocheza ligi saba za kina dada zilizo bora zaidi duniani kwa pamoja. (Guardian)

0 comments:

Post a Comment