Straika wa Manchester United, Romelu Lukaku hatatumikia
adhabu kwa kumchezea vibaya beki wa Brighton and Hove Albion Gaetan Bong
Jumamosi.
Chama cha Soka cha England (FA) kimeamua kutochukua hatua
zaidi dhidi ya mshambuliaji huyo kwa kushiriki kwenye tukio hilo dhidi
ya Bong.
Sekunde chache kabla ya Lewis Dunk kujifunga na kuipa United
goli la kuongoza katika ushindi wa 1-0 Old Trafford, Lukaku alionekana
akimpiga teke Bong baada ya kushindana ndani ya eneo la penalti.
Ripoti zilidai kuwa Lukaku angefungiwa kuichezea United
mechi tatu zijazo, ambazo zingekuwa ni pamoja na mechi dhidi ya Arsenal
na Manchester City.
Inaelewa kuwa Lukaku hataadhibiwa tena na FA kutokana na tukio hilo baada ya kuchunguzwa zaidi na waamuzi wawili wa mechi.
Kama ilivyo, Lukaku yupo huru kucheza mechi yake ya 200 Ligi Kuu YA England katika Vicarage Road.
Lukaku amefunga mabao 12 akiwa United katika michuano yote
tangu alipotua klabuni hapo akitokea Everton kwa pauni 75m, mechi ya
wikiendi ijayo Man united itakipiga dhidi ya Arsenal kisha Man City.
Home
»
»Unlabelled
» FA YAMSAMEHE LUKAKU ‘SASA KUZIVAA ARSENA NA MAN CITY’
Tuesday, November 28, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment