Wednesday, November 8, 2017



Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza watavaa vitambaa vyeusi katika mchezo wao wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Ujerumani Ijuma ya wiki hii.
Chama cha soka cha Uingereza kwa kushirikia na kile cha Ujerumani (DFB) vimethibitisha timu zote mbili kuvaa vitambaa hivyo kuungana na nchi hiyo katika kumbukumbu ya mashujaa waliyo kufa katika vita vya dunia.
Mwezi Septemba Bodi ya Kimataifa ya Shirikisho la Soka (IFAB) ilitoa mamlaka kwa timu ya nyumbani kuvaa vitambaa vyeusi ikiwa ni ishara ya kumbukumbu ya tukio la heshima.
Mkurugenzi wa chama cha soka nchini Uingereza, Martin Glenn  amesema watatumia mchezo huo kwa kuvaa vitambaa kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa waliyoweza kuisadia nchi hiyo.
Baada ya mchezo wa Ijumaa dhidi ya Ujerumani timu hiyo ya taifa ya Uingereza atashuka tena dimbani siku ya Jumatatu kuivaa Brazili.

0 comments:

Post a Comment