Liverpool walitoka suluhu ya bao 3 kwa 3 zidi ya Sevilla
ambapo Sevilla walitoka nyuma kwa bao 3 na kusawazisha, hii ni mara ya
kwanza kwa Liva kutangulia kwa idadi hiyo ya mabao na yakarudi tangu
itokee hivyo mwaka 2014.
Real
Madrid nao jana waliifunga jumla ya mabao 6 kwa nunge Apoel, hii
ilikuwa mara ya kwanza kwa Real Madrid kufunga mabao manne katika
kipindi cha kwanza katika michuano ya Champions League.
Lakini
Real Madrid hao hao usiku wa jana wameweka rekodi ya kuwa klabu ya
kwanza kushinda michezo 50 ya Champions League ugenini wakiwapiku
wapinzani wao Barcelona walioshinda michezo 49.
Manchester
City nao usiku wa jana waliendeleza rekodi yao nzuri ya ushindi baada
ya kuinyuka Feyenoord kwa bao 1 kwa nunge na sasa kwa mara ya kwanza
City wanakuwa wameshinda michezo 5 mfululizo ya Champions League.
Tottenham
nao hiyo jana walishinda mabao 2 kwa 1 na kujihakikishia nafasi ya
kwanza huku Harry Kane akifunga mabao 39 katika michezo 38 na kwa sasa
hakuna mchezaji aliyehusika katika mabao mengi UCL zaidi ya Kane (5
magoli na assist 2).
Home
»
FOOTBALL
» Matokeo unayajua, lakini hiki ndicho usichokijua kuhusu usiku wa Champions League hapo jana
Wednesday, November 22, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment