Tuesday, November 21, 2017

Facebook
Hakuna bata! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kukipangia kikosi chake programu ya kufanya mazoezi Siku ya Krismas kwenye Uwanja wa Old Trafford kutoka uwanja wao wa kawaida wa mazoezi, Carrington.
Mourinho, amewapangia programu hio mpya wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo wa Siku ya Kupeana Zawadi (Boxing Day) dhidi ya Burnley itakayoanza saa 11 jionii  ndani ya dimba hilo.
Maamuzi hayo ya kuhama Carrington, ndani ya Krismas yanatarajia kuwahusisha wafanyakazi wengine 50 au zaidi ambao watakua kwenye majukumu mbali mbali siku hio huku wakikosa kuutumia muda huo kujivinjari na familia zao.
Mazoezi ndani ya viwanja vya Carrington hujumuisha wafanyakazi 20 lakini kufuatia mabadiliko hayo, idadi ya wafanyakazi inatarajiwa kufikia hadi 70 watakaoshughulikia masuala mbali mbali ikiwemo ulinzi na uandaaji wa dimba hilo.

0 comments:

Post a Comment