Tuesday, November 21, 2017


KIUNGO mshambuliaji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Haruna Chanongo ameungana na wenzake kiuanza mazoezi baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje tangu mwanzo wa msimu.
Chanongo aliyeumia Mei mwaka huu na kutakiwa kuwa nje kwa miezi sita, ameanza na mazoezi mepesi aliyopangiwa na jopo la madaktari wa klabu ya Mtibwa Sugar na sasa madaktari wamemruhusu kutumika katika michezo ya kimashindano baada ya kufanya vipimo vya mwisho nakuonekana yupo fiti.
Maneja wa mabingwa hao mara mbili wa Ligi Kuu, 1999 na 2000, Sidy Ibrahim amesema kwamba taarifa ya jopo la Madaktari wa timu wakiongozwa na DK. Mussa Juma wamemruhusu Chanongo kuanza kucheza.
Haruna Chanongo ameungana na wenzake kiuanza mazoezi baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje tangu mwanzo Mei

“Chanongo ameruhusiwa kucheza hata michezo ya kimashindano baada ya kufaulu vipimo vya mwisho, hivyo hana tatizo lolote na mazoezi kafanya na wenzake na anaonekana kuwa fiti hivyo hata mchezo ujao anaweza kutumika kulingana na mahitaji ya kocha”alisema.
Nyota huyo hadi anaumia alikuwa katika kiwango bora katika klabu ya Mtibwa Sugar na alikuwa amefunga mabao saba katika michezo ya Ligi Kuu msimu uliopita.
Kurejea kwa Chanongo kunafanya nyota waliopona majeraha ya muda mrefu kufikia wawili katika kipindi hiki baada ya beki Hassan Isihaka aliyesajiliwa msimu huu kutoka African Lyon alipokuwa anacheza kwa mkoppo kutoka Simba naye kupona.
Baada ya kipigo cha jana cha 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar watakuwa wageni wa Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam  Novemba 27, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment