Mzimu wa kesi za ukwepaji kodi wazidi
Lioneil Messi, Javier Mascherano, Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho tayari waliingia matatani katika sheria za nchini Hispania, wote hao walikutwa na kesi inayohusu ukwepaji kodi nchini hapo.
Sasa kesi ya namna hiyo imeibuka kwa kiungo wa ushambuliaji wa klabu ya Real Madrid Luca Modric ambaye naye anadaiwa kutenda kosa hilo mwaka 2014 na mamlaka zinazohusiana na kodi za nchini humo zimeanza kumchunguza.
Katikati ya mwaka 2013 -2014 Modric alifanga tukio hilo na anadaiwa kukwepa kiasi cha £770,000 ambapo inadaiwa kwamba tukio hilo alilifanya kwa kushirikiana na mkewe
Habari za Luka Modric kukwepa kulipa kodi zinakuja masaa machache baada ya mlinzi wa kulia wa Real Madrid Marcelo kupanda kizimbani kujibu kesi kuhusiana na tukio kama hilo.
0 comments:
Post a Comment