Thursday, November 30, 2017


Hali ya kiungo mnyumbulikaji wa Arsenal Santiago Carzola inasikitisha sana, tumekuwa tukitaraji habari nzuri kutoka kwa madaktari wanaomtibu Carzola lakini taarifa iliyotoka inaumiza sana.
Ni mwaka na zaidi sasa kiungo huyo yuko nje ya uwanja na jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba ameshafanyiwa oparesheni nanw ili kutibu tatizo lake la mguu na mwezi ujao alipaswa kuanza mazoezi.
Lakini kupitia mtandao wake wa Twitter Carzola ametoa ujumbe ambao umewaumiza watu wengi, Carzola anasema bado anasikia maumivu katika mguu wake na hii inamfanya arudi tena hospitali kwa oparesheni ya tisa.
Matatizo yanayomkumba Carzola yanaonekana madogo kwa kuyazungumzia lakini watu wake wa karibu ikiwemo Arsene Wenger anasema ni majeruhi mabaya kuwahi kuyaona tangu aanze kufundisha soka.
Nahodha wa timu ya taifa Hispania Sergio Ramos amemtumia ujumbe Carzola wa kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu anachopitia na kusema kwamba dunia bado inahitaji kuona akitoa burudani ndani ya uwanja.

0 comments:

Post a Comment