Kati ya sababu ambayo imeshaanza kuongelewa kama chanzo cha kutofanya vizuri kwa Real Madrid msimu huu ni ukosefu wa penati, michezo 11 ya ligi kuu La Liga Los Blancos hawajapewa penati.
Mara ya mwisho kwa Real Madrid kucheza michezo 11 bila kupewa penati ilikuwa msimu wa mwaka 1980/1981 na kuanzia hapo Real Madrid wamekuwa wakipewa penati nyingi kula msimu.
Kuanzia msimu wa mwaka 1982 Real Madrid hawajawahi kucheza mechi 11 bila penati ambapo msimu uliopita katika kipindi kama hiki tayari Real Madrid walikuwa wameshapewa pigo la penati mara mbili.
Msimu wa mwaka 2015/2016 Real Madrid almanusra wakose penati lakini walifanikiwa kupata penati moja katika michezo 11 lakini msimu wa 2014/2015 ndio waliweka rekodi kwani walipata penati 5 katika mechi 11.
Kuanzia msimu wa 2011/2012 hadi kufikia msimu wa mwaka 2014/2015 Real Madrid hawajawahi kupewa chini ya penati 4 ndani ya mechi 11 za mwanzo na wakipata penati 19 katika misimu minne mechi 11 za mwanzo.
Tangu Cristiano Ronaldo ajiunge na Real Madrid mwaka 2009 hawajawahi kukaa muda mrefu hivi bila kupata penati na sasa ukame wa mabao unaomuandama Cr7 unatajwa kusababishwa na ukame wa penati.
0 comments:
Post a Comment