Wanariadha wengine
watano wa Urusi wamefungiwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Olimpiki
kwa maisha yao yote baada ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuwabaini
kutumia dawa zilizokataliwa michezoni.
Sergei Chudinov, Aleksei Negodailo, Dmitry Trunenkov, Yana Romanova na Olga Vilukhina ndio waliokumbwa na adhabu hiyo.IOC inasema kufungiwa huko kunatokana na kamati ya 2016 ya McLaren iliyoonyesha watumiaji wa dawa hizo.
Siku ya Jumatatu IOC ilitangaza adhabu hiyo na kuonya kuwa bado itaendelea kwa wale wote watakaojaribu kutumia dawa hizo.
0 comments:
Post a Comment