Mshambuliaji wa
Arsenal Alexis Sanchez haonekani kuimarika na huenda kiwango chake cha
mchezo 'kimeisha', kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian
Wright.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefunga mabao manne
katika ligi ya Uingereza msimu huu ikiwa ni mabao manane chini ya muda
kama huo msimu uliopita.Sanchez ambaye alihusishwa na klabu ya Manchester City mapema mwaka ujao atakamilisha kandarasi yake na Arsenal mwishoni mwa msimu huu.
Vile anavyosakata soka, sioni vile atakavyoathiri Arsenal, Wright aliambia BBC radio 5 moja kwa moja.
Sanchez ameifungia Arsenal mara 77 tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Barcelona 2014.
Wright ambaye aliifungia Arsenal mara 185 katika mechi 288 haamini kwamba mshambuliaji huyo wa Chile 'anafanya bidii'.
Amesema: Watu wanaotafuta kununua wachezaji wanafikiria nini kumuhusu yeye na tabia yake?
Kama Sanchez , kiungo wa kati Mesut Ozil pia anakamilisha kandarasi yake mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alifunga bao la pekee siku ya Jumamosi dhidi ya Newcastle, na alitengeza nafasi nane za mabao.
Lakini Wright hana matumaini kwamba raia huyo wa Ujerumani atasalia. ''Ningependa kukosolewa'', alisema.
Kile tunachoona kutoka kwake sasa ndio mchezo ambao tumekuwa tukitaka kuuona kutoka kwake.
0 comments:
Post a Comment