Bingwa wa mchezo wa
tenisi duniani upande wa wanawake Serena Williams huenda anakabiliwa na
changamoto kubwa baada ya kuwataka mashabiki wake katika mitandao ya
kijamii kumshauri vile atakavyokabiliana na tatizo la mwanawe wa kike
anayeanza kuota meno.
''Tatizo la mwana anayemea meno ni gumu kutatua'', aliwaambia.Anasema kuwa ametumia kila njia ikiwemo taweli za baridi mbali na kumpatia mwanawe kidole chake akisema kuwa alimbeba mwanawe hadi aliposhikwa na usingizi.

Mwanawe wa kike Alexis Olympia Ohanian Jr alizaliwa mnamo tarehe mosi mwezi Septemba
Mashabiki wa Serena nao walikuwa na ushauri tofauti kwake.
Wengi walimtaka kung'ata wanaserere matunda baridi ama hata barafu.

Kulikuwa na mapendekezo ya kutumia maziwa ya mama iwapo anaendelea kunyonya ama hata kumnyonyesha kama njia moja ya kupunguza tatizo

0 comments:
Post a Comment