DAVID Silva, nyota wa Manchester City amecheza jumla ya mechi 400 tangu ajiunge na kikosi hicho msimu wa mwaka 2010.
Anakuwa mchezaji wa 14 kufikia idadi ya michezo hiyo ndani ya Manchester City na mtu wa mwisho alikuwa ni Paul Power ambaye alicheza jumla ya michezo 445.
Silva amekuwa imara ndani ya City na ametwaa mataji manne ya Ligi Kuu England, mataji mawili ya FA, mataji manne ya League Cup na Ngao mbili za jamii .
Rekodi zake ndani ya Premier League amepiga jumla ya assisti 83 na ametengeneza jumla ya nafasi 745 na amekuwa bora Kwa muda mrefu.
Jana City iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Bournemouth, mabao yao mawili yalifungwa na Sergio Arguero na moja likipachikwa na Raheem Sterling aliyepachika moja na la kufutia machozi kwa Bournemouth ni Harry Wilson.
0 comments:
Post a Comment