Thursday, August 29, 2019


Uefa leo Alhamisi inatarajiwa kumtangaza mchezaji bora wa mwaka wa soka Barani Ulaya . Waliojumuishwa katika orodha ya kushindania tuzo hiyo ni beki ya Liverpool Virgil van Dijk anawania taji hilo dhidi ya Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi Barcelona. Kama Luka Modric alivyofanikiwa kuwaoondoa Ronaldo na Messi katika udhibiti wa tuzo hiyo mwaka jana nae Van Dijk ana matumaini ya kuwapiku nyota hao wa soka kwa kuishindia Liverpool taji hilo mashuhuri. Lakini wachezaji hao watatu wameonesha umahihiri wao kiasi gani uwanjani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita?

Messi na Ronaldo Mahasimu wa jadi wakutana tena
Ni ushindani ambao umeaanza kitambo sana na kila mmoja anajua hilo. Linapokuja suala la kuorodhesha wachezaji bora wa kuwania mataji – iwe ni Barani Ulaya au Duniani- Messi na Ronaldo wamejumuishwa katika orodha hizo kwa zaidi ya mwango mmoja. Tangu Tuzo ya Uefa ya mchezaji bora wa kiume ilipozinduliwa mwaka 2011, Ronaldo ameshinda mara tatu (2014, 2016, 2017), huku Messi akishinda Tuzo hiyo mara mbili (2011 na 2015). Wawili hao wanamenyana tena baada ya misimu ya kusisimua ya. Ronaldo aliisaidia Juventus kushinda ligi ya Italia maarufu Serie A nae Messi akaongoza Barcelona kushida ligi ya La Liga . Lakini takwimu uwanjani zinaonesha wachezaji hao wawili walifanya vipi mwaka mmoja uliopita?

Lionel Messi

Cristiano Ronaldo


BarcelonaArgentinaKlub & nchiJuventusUrenoKlabu & nchi
Meche zilizochezwa5085843447
Dakika zilizochezwa4,0246224,6463,6463003,946
Magoli5135428331
Goli kwa dakika7920786130100127
Jumla ya mabao2582628423519254
mabao yaliowekwa kimyani19.8%11.5%19%11.9%15.8%12.2%
Magli yaliotarajiwa (xG)35.623.3138.9328.31.2929.59
*Takwimu yote ni ya kutoka Julai 31 2018 hadi Julai 31 2019





Kati ya tarehe 31 mwezi Julai 2018 na tarehe 31 mwezi Julai mwaka 2019, Messi alikuwa mshambuliaji hatari katika klabu yake na nchi yake. Katika kipindi hicho cha miezi 12 alifunga mabao 54 ikilinganishwa na mabao 31 ya Ronaldo na kuongeza takwimu ya mabao kwa kila dakika ya 86, ikilinganishwa 127 ya hasimu wake wa Ureno. Messi pia alifanya vizuri zaidi yaalivyotarajia alipopata nafasi ya kufungia mabao Barcelona. Ronaldo, wakati huo alifunga mabao 28, kama alivyotarajia.

Alifanya vizuri zaidi akilinganishwa na wachezaji wengine wa Ulaya, Messi alifunga mabao zaidi ya mahasimu wake – wa karibu zaidi ni mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, aliyefunga mabao 11 ikilinganishwa na mabao 40 yaliofungwa na nyota huyo wa kimataifa wa Argentina. Ronaldo, alishidwa na wachezaji wanane katika ufungaji wa mabao katika ligi tano kuu za ulaya huku mabao 21 alizofunga katika ligi hizo zilishindwa na wachezaji watatu wa ligi ya Serie A.

Huwezi kuchenga na kumpita

Virgil Van Dijk
Image captionSiku ya Jumamosi, Nicolas Pepe wa Arsenal alikuwa mchezaji wa kwanza kumchenga Virgil van Dijk
Van Dijk amekuwa baraka kwa Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Southamptonna ammekuwa kiungo muhimu kuisaidia kushinda Champions League msimu uliopita na pia kuisaidia kuwania taji ya Ligi ya Premia dhidi ya Manchester Cityhadi mwisho. Beki huyo hajawahi kushinda tuzo kwa hivyo hatua ya nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi kuwania tuzo dhidi ya Messi na Ronaldo tayari ni mafanikio makubwa.

Lakini je ana nafasi ya kuvikwa taji la mchezaji bora Barani Ulaya?
Takwimu za michezo mwaka 2018-19 zinaonesha Van Dijk aliiwakilisha klabu na taifa lake katika mechi 59 msimu uliopita. Alifunga mabao tisa na kusaidia ufungaji wa mabao manne. Pia alichezea Liverpool kwa dakika nyingi zaidi (4,465) ya mchezaji mwingine yeyote. Katika mashindano yote ameonesha kwa zaidi ya 70% umuhimu wake kama beki.
Virgil van Dijk

LiverpoolNetherlandsClub & Country
Meche zilizochezwa50959
Dakika zilizochezwa4,4658405,305
Duels41164475
Duels zilizoshindwa30347350
Ufanisi wake %73.7%73.4%73.7%
Ulinzi30844352
ulinzi ulioshindwa22334257
Ufanisi wa ulinzi %72.4%77.3%73%
Liverpool ilifungwa mabao machache(22) tikilinganishwa na vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita na Van Dijk alichangia ufanisi huo kwa 76.3%. Ukimlinganisha Van Dijk na mabeki wengine wa Ligi tano kubwa Ulaya mchezaji huyo aliongoza katika msimu wa 2018-19 kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo.
Mabeki wa ligi tano kuu Ulaya: 2018-19CompetitionDuelsDuels WonDuels Success
Virgil van DijkLigi Kuu ya Uingereza32124576.3%
MarceloLigue 1 ya Ufaransa32523772.9%
Harry MaguireLigi Kuu ya Uingereza24918172.7%
Salif SanéBundesliga ya Ujerumani30721971.3%
Shane DuffyLigi Kuu ya Uingereza34023870.0%
Hii ndio sababu kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekuwa akimsifia mchezaji huyo baada ya klabu hiyo kuinyuka Arsenal mabao 3-1 siku Jumamosi iliyopita, lakini meneja huyo wa zamani wa Borussia Dortmund anahisi wakati umewadia kwa beki huyo kutambuliwa kama mchezaji bora wa soka Ulaya. “Soka ya kisasa inatakiwa kuwa wazi kwa vitu kama hivi,” alisema. “Hatuhitaji kuzungumzia Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Kama tuliwazungumzia msimu uliopita, Virgil anastahili tuzo; lakini kama tunazungumzia taaluma ya maisha Messi na Ronaldo wapigania tuzo hilo

0 comments:

Post a Comment