Arsenal ilicharazwa mabao 3-1 na Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield, wikiendi iliyopita huku mabao mawili yakiwa yametokana na makosa ya Luiz.
Beki huyo alisababisha penalti iliyozaa bao la pili baada ya kumvuta straika wa Liverpool, Mohamed Salah. Pia Luiz alipigwa chenga na Salah, ambaye pia alimzidi mbio na kupachika bao la tatu katika mchezo ule. Kilikuwa kipigo cha kwanza kwa Arsenal msimu huu, ambapo Luiz alikiri wanapaswa kufanyia kazi mapungufu yao kwenye safu yao ya ulinzi.
“Ni ukweli ulio wazi tunatakiwa kufanyia kazi tatizo hili la kuruhusu mabao mengi. Huwezi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England wakati beki yako inafungwa ovyo,” aliongeza Luiz, ambaye timu yake ya Arsenal ilifungwa mabao 51 kwenye msimu uliopita wa 2018/19.
0 comments:
Post a Comment