Cristiano Ronaldo akiwa ameshika tuzo ya Ballon d'Or baada ya kukabidhiwa leo mjini Paris, Ufaransa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or mwaka 2017.
Ronaldo ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya tano katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Eiffel Tower akiwaangusha Muargentina Lionel Messi na Mbrazil Neymar.
Ronaldo
anayechezea Real Madrid sasa analingana na Messi wa Barcelona, zote za
Hispania kwa kutwaa mara nyingi zaidi Ballon d'Or, kila mmoja mara tano.
Na mafanikio yake yanafuatia kuiwezesha Real Madrid kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga msimu uliopita wa 2016-17.
Mshindi
wa 2017 ametajwa kwa mbwembwe za aina yake, akitokea kwenye video
ukumbi wa Eiffel Tower na akaonekana Ronaldo amesimama akiwa ameshika
tuzo yake.
"Ndiyo,
najisikia furaha. Ni wakati mzuri katika maisha yangu," amesema Ronaldo
wakati anakabidhiwa tuzo. Ni kitu fulani natumai kushinda kila mwaka.
Nawashukuru wachezaji wenzangu wa Real Madrid. Na ninataka kuwashukuru
watu wengine walionisaidia kufikia kiwango bhiki,".
Ronaldo
mwenye umri wa miaka 32, ambaye baadaye alifuatwa na mama yake, Maria
Dolores dos Santos Aveiro na mtoto wake wa kioume mkubwa, Cristiano
Ronaldo Jr huku mpenzi wake, Georgina Rodriguez akitazama kutoka eneo la
watu.
Ronaldo
ameshinda tuzo hiyo inayoandaliwa nchini Ufaransa baada ya kuwabwaga
wachezaji wengine 29 kutokana na kura za kikundi cha Waandishi wa Habari
173.
Messi
ameshika nafasi ya pili, kwa mara ya saba wawili hao wakishika nafasi
mbili za mwanzo za Ballon d'Or katika ushindani wao na Neymar amekuwa wa
tatu.
George Weah anabaki kuwa Mwafrika pekee aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 1995 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
George Weah anabaki kuwa Mwafrika pekee aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 1995 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment