Tuesday, August 20, 2019


Baada ya club ya Man United kupokea vipigo mara mbili mfululizo kutoka kwa Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu na Kombe la FA msimu uliopita, leo walikuwa ugenini kuifuata Wolves kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi yao, Man United walikuwa wageni na wengi walitamani kuona watafanya nini cha ajabu.
Man United wakiwa ugenini wamejikuta wakiambulia sare ya kufungana goli 1-1, Man United ndio walikuwa wa kwanza kuandika goli dakika ya 27 kupitia kwa Anthony Martial lakini Wolves kaja kuchomoa dakika ya 55 kupitia kwa Ruben Neves na kuifanya Man United kushindwa kupata nafasi ya kuongoza Ligi, kwani ushindi wa aina yoyote leo ungewafanya waongoze Ligi kwa tofauti ya magoli.

Mara ya mwisho kwa Man United kumfunga Wolves ilikuwa March 18 2012 katika mchezo wa Ligi Kuu England ambapo Man United walipata ushindi wa magoli 5-0, kwa ujumla Man United na Wolves wamewahi kukutana mara 102, Wolves akishinda mara 36 na Man United mara 48 huku sare ikiwa 18.

0 comments:

Post a Comment