Manchester
United inamatumaini ya kumsajili kinda wa klabu ya Borussia Dortmund,
Jadon Sancho katika dirisha la usajili majira ya joto, huku miamba ya
soka ya Ujeruman ikiwa imeanza. (Metro)
Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, huuenda akaondoka klabu hiyo msimu wa majira ya joto. (Sun)
Monaco wanamtaka mshambuliaji wa Uingereza Daniel Sturridge, 29, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Liverpool. (L’Equipe in French)
Kiungo wa kati Mswizi Xherdan Shaqiri, 27, amesema anatafakari hatma yake ya baadae Liverpool ikiwa hatapewa nafasi ya kutosha ya kucheza. (Langenthaler Tagblatt via Daily Star)
Kumkosa mshambuliaji wa England r Harry Kane, 26, huenda kukaiathiri Tottenham ikilinganishwa na kukpoteza huduma ya Christian Eriksen, 27, anasema beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher. (Daily Telegraph)
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ameelezea furaha yake kuwa James Rodriguez, 28, katika kikosi chake licha ya mchezaji huyo raia wa Colombia hivi karibuni kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Bernabeu. (Corriere dello Sport – in Italian)
Ndungu ya Paul Pogba, Mathias anasema kuwa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa wa miaka 26, bado anataka kuondoka Manchester United na kujiunga na Real Madrid. (El Chiringuito via Daily Mail)
Meneja wa Celtic Neil Lennon anasisitiza kuwa hana mpango wa kumnunua kipa mpya msimu huu. (Daily Record)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 33, ametia saini kandarasi mpya ya miaka mitatu na klabu ya Roma, licha ya tetesi kuibuka huenda akajiunga na mahasimu wa klabu hiyo Inter Milan. (AS Roma)
Winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 21, amabye analengwa na Bayern Munich na Manchester United amethibitishia PSV Eindhoven uaminifu wake kwa klabu hiyo baada ya kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano. (Goal)Neymar
Kocha wa Brazil Tite anasema Neymar, 27, anasubiri Paris St-Germain imfanyie uamuzi kuhusu hatma yake ya baadae. (Marca)
Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa hana uhakika ikiwa usajili wa wachezaji wapya umeimarisha kikosi cha Gunners. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Tottenham Moussa Sissoko anasemekana kuangua kilio baada ya kushindwa katika fainali ya Champions League na Liverpool.(Talksport)
Haki miliki ya Moussa Sissoko amecheza mechi zote za Tottenham katika Ligi ya Premia miaka minne iliopita
Tetesi Bora Ijumaa
Meneja wa United, Ole Gunnar Solskjaer amefanya mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham, Christian Eriksen kuhusu uwezekano wa uhamisho kuelekea Old Trafford, hatahivyo mchezaji huyo wa miaka 27alikuwa anataka kusubiria uhamisho kuelekea Uhispania. (Manchester Evening News)
Beki wa kati wa England Harry Maguire, mwenye miaka 26, amekataa pendekezo la thamani ya £278,000 kwa wiki kutoka Manchester City badala ya kujiunga na timu hasimu United. (Star)
Napoli imekataa ombi la thamani ya £82m kutoka kwa Manchester United kwa mchezaji wa miaka 28 raia wa Senegal Kalidou Koulibaly kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho England. (Corriere dello Sport, kupitia Calciomercato)
Winga wa Bournemouth Jordon Ibe anasakwa na mabingwa wa Uskotchi, Celtic. Timu ya Napoli Italia, tayari imemuulizia mchezaji huyo wa miaka 23. (Sun)
Juventus bado inatumai kumuondoa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Argentina, Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho Ulaya – licha ya kwamba mabingwa hao wa Italia bado hawajapokea maombi thabiti kwa mchezaji huyo. (Independent)
0 comments:
Post a Comment