Manchester United imetangaza kumsajili mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka Arsenal, zote za England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU
ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Alexis
Sanchez kwa mkataba wa miaka minne na nusu kutoka Arsenal na Henrikh
Mkhitaryan anakwenda upande wa pili.
Akiuzungumzia
uhamisho wake, Alexis Sanchez amesema: "Nina furaha kujiunga na klabu
kubwa duniani. Nimekuwa Arsenal kwa miaka mitatu na nusu mizuri na
imenipa kumbukumbu nzuri klabu hiyo kubwa na mashabiki wake.
"Nafasi
ya kucheza kwenye Uwanja huu wa kihistoria na kufanya kazi na Jose
Mourinho ni ambayo nisingeweza kuikataa. Ninayo furaha kuwa mchezaji wa
kwanza wa Chile kuchezea timu ya kwanza ya United na ninatumai ninaweza
kuwaonyesha mashabiki wetu dunia nzima kwa nini klabu imenileta hapa,".
Jose
Mourinho kwa upande wake amesema: "Alexis ni mmoja wa washambuliaji
bora duniani na tutakamilisha safu yetu ya ushambuliaji ya wachezaji
chipukizi na wenye vipaji. Ataleta matarajio yake, dhamira na haiba,
sifa ambazo zimemfanya awe mchezaji wa Manchester United na mchezaji
ambaye anaifanya timu iwe madhubuti na mashabiki wajivunie timu yao,".
"Ningependa
kumtakia kila la heri Henrikh, mafanikio yote na furaha ambayo nina
uhakika anakwenda kuipata. Ni mchezaji ambaye hatutamsahau, hususan
kutokana na mchangi wake kwenye ushindi wa taji letu la Europa
League,"amesema.

0 comments:
Post a Comment