Monday, January 22, 2018

Javi Gracia,kocha mpya Watford


Klabu ya Watford imemtangaza Javi Gracia kuwa kocha mpya wa timu hiyo,baada ya kumtimua kocha wa zamani Marco Silva.
Kocha huyo mpya raia wa Hispania amesaini mkataba wa miezi 18,na hiki ni kibarua chake kingine tangu aachane na kazi ya kuinoa klabu ya Rubin Kazan mwezi June mwaka jana.
Kocha huyu mwenye miaka 47 alidumu misimu miwili ya ligi ya Hispania La Liga na pia alifanya kazi nchini Ugiriki.
Gracia anakuwa kocha wa 10 kufanya kazi ya kukinoa kikosi hiki cha Watford chini ya familia ya Pozzo tangu mwaka 2012.

0 comments:

Post a Comment