Mourinho alikuwa KOCHA BORA NA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA klabuni Man Unted katika msimu wake wa kwanza kitu ambacho hakuna kocha mwingine ambaye amewahi kufanya hivyo hapo awali.
Msimu wake wa kwanza aliweza kutwaa kombe la EFL kiwanjani Wembley mwezi Februari, pia alitwaa kombe ambalo hakuna kocha mwingine aliwahi kulinyakua katika historia ya klabu nalo ni kombe la Uropa jijini Stockholm Ubelgiji.
Mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Bw. Ed Woodward amesema kuwa, “jose mourinho tayari ameshapata mafanikio makubwa klabuni hapo, hakuna shaka juu ya uwezo wake, na hatuna haja ya kuendelea kuweka kizuizi juu ya mkataba mpya. UWEZO WAKE NA UJUZI WAKE, NA HAMU YAKE YA KUINUA VIPAJI CHIPUKIZI KATIKA KIKOSI CHA KWANZA ni moja ya vitu ambavyo vilikuwa kwenye malengo makuu ya klabu hii. Ameongeza hari kubwa na motisha kwa mashabiki na klabu kwa ujumla”.
Mourinho pia amesema “ni heshima ya pekee n aya kujivunia kuwa kocha mkuu wa Man United. Natamani kufikisha salamu zangu za dhati na shukrani kwa mashabiki wote wa united, mabos wa klabu hii kwa kutambua kazi yangu na umuhimu wangu klabuni hapa, nina furaha kubwa kusema kitendo cha wao kutambua uwezo wangu na nafasi yangu katika klabu hii ni jambo la kheri. Na nina uhakika mimi ndiye KOCHA SAHIHI YA KLABU KUBWA HII YA MAN UNITED.
Tunaweka mipango murua na endelevu, nina uhakika tuna kila sababu ya kupigania na kushinda MAKOMBE MATATU MSIMU HUU. Tunahakikisha tutajenga Manchester united bora na kubwa zaid kwa siku za sasa na siku zijazo.nashukuu ofisi nzima na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote na mashabiki wote kwa ujumla KWA MOTISHA NA MUDA WAO WANAOJITOLEA KWA JAILI YA MANCHESTER.
0 comments:
Post a Comment