JESHI la Polisi mkoani Kagera, limesema
bado linaendelea kumshikilia beki wa kati wa Kagera Sugar, Juma Nyoso,
anayetuhumiwa kumpiga shabiki anayedaiwa kuwa wa Simba, Shaaban Hussein,
mkazi wa Kemondo, Bukoba.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini
hapa, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi, Issack Msengi, alisema jeshi hilo linaendelea kumshikilia Nyoso,
kutokana na majeruhi kutojitambua hadi sasa.
“Hadi sasa tunamshikilia Nyoso kwa sababu
majeruhi bado hajajitambua na bado amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Kagera katika wodi namba moja, na leo hii (jana), tumetuma
mpelelezi wetu amerudi bila maelezo yoyote” alisema.
Msangi alisema kuwa dhamana kawaida
inazingatia mazingira na hali ya majeruhi, na kuwa kwa sasa majeruhi
huyo bado hajaongea kwa hiyo jeshi hilo halijapata taarifa yoyote kutoka
kwake.
“Kwa mujibu wa taarifa za awali za Nyoso,
alidai siyo yeye aliyempiga shabiki huyo na kuwa alipigwa na mwenzake,
kwa hiyo yeye (majeruhi) akizungumza ndiye atamtaja aliyempiga ni nani”
alisema.
Alisema kuwa majeruhi akishahojiwa ndipo
itafahamika hatua zinazofuata kwa Nyoso ni zipi, na kuwa hawezi kusema
kuwa watampeleka mahakamani kwa kuwa ili kesi iende mahakamani, lazima
uwapo ushahidi unaojitosheleza kutoka hata kwa watu wengine waliokuwapo.
“Nyoso anaweza akafikishwa mahakamani au
asifikishwe kutegemeana na ushahidi utakaopatikana, lakini pia maelezo
ya majeruhi kuthibitisha kuwa ndiye aliyempiga,” alisema Mrakibu huyo
mwandamizi wa polisi.
Juzi, Jumatatu, baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, wakati
wachezaji wa timu ya Kagera Sugar
wakiondoka uwanjani, shabiki huyo anayedaiwa kuwa ni wa Simba kutokana
na mavazi yake, aliwafuata wachezaji wa timu ya Kagera Sugar akiwamo
Nyoso na kuanza kuwazomea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Augustine Ollomi, baada ya tukio hilo,
shabiki huyo alimpulizia vuvuzera Nyoso, hivyo kusababisha kushambuliwa.
Katika mchezo huo, Simba inayodhaminiwa na
Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, iliibuka na
ushindi wa mabao 2-0, yaliyofungwa na Said Ndemla na nahodha John Bocc
0 comments:
Post a Comment