Mshambuliaji
wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann akisikitika baada ya kupoteza
nafasi ya kufunga usiku wa jana Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan
wakifungwa 3-1 na wenyeji Sevilla katika mchezo wa marudiano wa Robo
Fainali ya Kombe la Mfalme na kutolewa kwa jumla ya mabao 5-2 kufuatia
kufungwa pia 2-1 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani kwao. Mabao ya Sevilla
yalifungwa na Sergio Escudero dakika ya kwanza, Ever Banega dakika ya
48 na Pablo Sarabia dakika ya 79, wakati la Atletico lilifungwa na Griezmann dakika ya 13
Home
»
»Unlabelled
» GRIEZMANN HOI, ATLETICO YANG'OLEWA KOMBE LA MFALME
Wednesday, January 24, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment