Mshambuliaji Sergio Aguero akishangilia na mchezaji mwenzake, Bernardo Silva baada ya kuifungia bao la pili dakika ya 49 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji, Bristol-City
kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu
kama Carabao Cup Uwanja wa Ashton Gate usiku wa jana. Mabao mengine ya
City yalifungwa na Leroy Sane dakika ya 43 na Kevin De Bruyne dakika ya
90 na ushei wakati mabao ya Bristol yamefungwa na Marlon Pack dakika ya
64 na Aiden Flint dakika ya 90 na ushei kabla ya bao la tatu la
washindi. Man City inakwenda fainali ya Kombe la Ligi kwa ushindi wa
jumla wa 5-3 baada ya kushinda 201 nyumbani kwenye mchezo wa kwanza na
sasa itakutana na mshindi kati ya Arsenal na Chelsea
Home
»
»Unlabelled
» MANCHESTER CITY YATANGULIA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND
Wednesday, January 24, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment