Mchezaji
aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na Barcelona Ousmane Dembele huenda
akarejea kucheza wiki hii baada ya kukaa nje ya uwanja wa karibu miezi
minne.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye miaka 20 alijiunga na
Barca Agosti kwa £96.8m lakini akaumia akichezea klabu hiyo mechi yake
ya tatu - dhidi ya Getafe mnamo 16 Septemba.Dembele alifanyiwa upasuaji nchini Finland.
Sasa, huenda akarejea kucheza dhidi ya Celta Vigo katika Copa del Rey Alhamisi.
Viongozi wa ligi Barcelona kisha watakutana na Levante katika La Liga Jumapili.
Barca ambao wamo alama tisa mbele kileleni kwenye ligi wamepangiwa kukutana na Chelsea hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Februari na Machi.

Pesa walizolipa Barcelona mwanzoni zilikuwa karibu nusu ya £200m walizopokea kutoka Paris St-Germain kwa mshambuliaji Mbrazil Neymar.

0 comments:
Post a Comment